Mheshimiwa Dkt. Habib Kambanga, Balozi wa Tanzania nchini Rwanda amelipongeza Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa kuendelea kuwa kiungo muhimu katika kuimarisha kwa ushirikiano baina ya Tanzania na Rwanda. Balozi Kambanga ameeleza kuwa Ubalozi wa Tanzania nchini Rwanda unafurahishwa na ushirikiano mzuri uliopo baina ya majeshi ya Tanzania na Rwanda katika kikao chake na ujumbe wa JWTZ ambao upo nchini Rwanda kwa ziara ya kikazi.


