Mheshimiwa Dkt. Habib Gallus Kambanga, Balozi wa Tanzania nchini Rwanda amekutana na kufanya mazungumzo na timu ya mbio za magari Asas ambayo imewasili nchini Rwanda kwa ajili ya kushiriki katika mashindano ya mbio za magari ya Afrika (Africa Rally Championship) yatakayohusisha nchi 17 za Afrika. Timu hiyo imekuwa ikishiriki katika mashindano hayo katika nchi mbalimbali za Afrika ambapo kwa mwaka 2025 mashindano hayo yalifanyika Uganda na timu hiyo kushika nafasi ya kwanza. Mashindano hayo hufanyika kwa mzunguko ambapo mwezi Septemba 2026 yatafanyika Tanzania.




