Rais wa Jamhuri ya Muungao wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ashiriki katika mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali kuhusu Uvumbuzi wa Nishati ya Nyuklia barani Afrika (NEISA) unaofanyika Jijini Kigali kuanzia tarehe 19-21 Mei, 2026 katika ukumbi wa mikutano wa KCC. Mkutano huo wa kimtaifa unawakutanisha pia wataalamu wa nishati, wawekezaji na mashirika ya Kimataifa ambao utajadili matumizi ya nishati ya nyuklia kwa maendeleo ya Bara la Afrika. Aidha, Mkutano huo pia unalenga kujadili namna bora ya kuongeza upatikanaji wa nishati ya umeme Afrika, kupunguza uchafuzi wa mazingira, kusaidia maendeleo ya viwanda, kukuza ubunifu wa teknolojia ya nyuklia pamoja na kuvutia wawekezaji katika miradi ya nishati





