Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Mahmoud Thabit Kombo  akiambatana na Wajumbe wengine kutoka Tanzania wanahudhuria Kongamano la Nne la Sayasi, Teknolojia na Ubunifu la Jumuiya ya Afrika Mashariki (4th EAC Regional Science, Technology and Innovation Conference) iliyoandaliwa na Kamisheni ya Sayansi na Teknolojia ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EASTECO) kwa kushirikiana na Baraza la Vyuo Vikuu vya Jumuiya ya Afrika Mashariki (IUCEA) linalofanyika kuanzia tarehe 30 Machi 2026  hadi tarehe 01 Aprili, 2026 jijini Kigali,  Rwanda.  Kongamano hilo limewakutanisha Viongozi wa ngazi za juu Serikalini kutoka nchi Wanachama wa EAC, Wabunifu, Wanataaluma, Wanadiplomasia na Wadau wa maendeleo.