Mheshimiwa Dkt. Habib Kambanga, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Rwanda amekutana na kuzungumza na timu ya wataalam ambayo imefanya ziara nchini Rwanda kwa lengo la kujifunza kuhusu mfumo wa usimamizi wa usafiri wa pikipiki. Timu hiyo inajumuisha wataalam kutoka Wizara ya Uchukuzi na Wizara ya Mambo ya Ndani na itakutana na kufanya vikao na Wizara ya Usafirishaji ya Rwanda, Rwanda Utilities Regulatory Authority (RURA), pamoja na kampuni zinazosimamia mauzo na uendeshaji wa pikipiki zinazotumia umeme.  Akizungumza wakati wa kikao hicho Mheshimiwa Balozi Kambanga amesisitiza umuhimu wa timu hiyo kuhakikisha masuala watakayojifunza yanatekelezwa katika ngazi ya taasisi zinazohusika pamoja na nidhamu katika utii wa sheria za matumizi ya barabara.