Mheshimiwa Dkt. Habib Kambanga, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Rwanda amekutana na kuzungumza na timu ya wataalam ya wataalam kutoka Wakala wa Barabara za Taifa Tanzania (TANROADS) ambao wapo nchini Rwanda kwa ajili  ya kushiriki warsha iliyoandaliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (Africa Development Bank-AfDB) kuhusu usimamizi wa mikataba. Katika mazungumzo husika, Mheshimiwa Balozi Kambanga ameusisitiza ujumbe huo kutumia fursa hiyo kujifunza kutoka kwa nchi mbalimbali kuhusu ujenzi, usimamizi na uendelezaji wa barabara kwa ajili kukuza maendeleo.Vile vile, amegusia umuhimu wa TANROADS katika uendelezaji wa miundombinu na ukuaji wa biashara ya usafirishaji na bandari katika nchi mbalimbali zinazotuzuguka.