Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano nchini Rwanda umeshiriki katika Maonesho ya Pili ya Hisani ya Kidiplomasia yaliyofanyika  kwenye Ukumbi wa Mikutano na Maonesho wa Kigali (Camp Kigali). Lengo la maonesho hayo ni kuwezesha nchi mbalimbali zenye uwakilishi nchini Rwanda kuonesha bidhaa na huduma  mbalimbali zinazozalishwa/zinazotolewa na nchi husika pamoja na mila na desturi.  Ubalozi umetumia fursa hiyo kunadi vitabu na kamusi za Lugha ya Kiswahili, mavazi, vyakula na vinywaji vya Kitanzania, vivutio mbalimbali vya utalii na diplomasia ya uchumi kwa kuonesha na kuzungumzia shughuli zinazofanya na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Shirika la Ndege (Air Tanzania) pamoja na bidhaa zinazozalishwa na kampuni za Tanzania zinazowekeza  nchini Rwanda pamoja na zile zinazouza bidhaa  nchini humo.

Nchi nyingine zilizoshiriki katika maonesho hayo ni pamoja Urusi, Kenya, Ethiopia, Nigeria, Ghana, Angola na Uganda. Maonesho hayo pia yamehudhuriwa na wafanyabiashara wadogo na wa kati wanaozalisha na kuuza bidhaa/huduma mbalimbali nchini Rwanda.