Balozi wa Tanzania nchini Rwanda Mheshimiwa Mej. Jen. Ramson Godwin Mwaisaka, leo tarehe 22 Agosti, 2024, amekutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Twiga Cement Bw. Vyes Mataigne (Head of Commercial Cluster, East, South and Centre Africa) na Bw. Davis Tery (Commercial area Manager).  Twiga Cement ni kampuni ya Kitanzania ambayo ni miongoni mwa wauzaji wakubwa wa Saruji nchini Rwanda.  Mazungumzo yao yamejikita kwenye changamoto na namna ya kuboresha biashara ya saruji katika soko la Rwanda.