Tarehe 06 -07 Julai, 2025 Ubalozi  ulishiriki Maadhimisho  ya Kilele cha Sherehe za Siku ya Kiswahili Duniani kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliyoandaliwa na Serikali ya Rwanda, Maadhimisho hayo yalifanyika katika hoteli ya Serena, Kigali.  Waheshimiwa Mawaziri, Waheshimiwa Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Mkuu, Wakurugenzi na Mabaloz walishiriki  katika kilele hicho. Sherehe hizo zilizofana na zilipambwa kwa shughuli mbalimbali zikiwemo ngoma, mashairi, uzinduzi wa vitabu vya kiswahili, hotuba za viongozi mbalimbali pamoja na mabanda ya maonesho ya shughuli mbali mbali. Kama kawaida timu ya Tanzania ilichangia kuchangamsha sherehe hizo.