Mhe. Mej. Jen. Ramson Godwin Mwaisaka, Balozi wa Tanzania Nchini Rwanda amekutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Kampuni ya Primia Enterprise kutoka Zanzibar inayojishughulisha kuuza bidhaa za vyakula ikiwemo mafuta ya kupikia (Mico Gold), Kampuni hiyo imefungua Kampuni nyingine nchini Rwanda (Pamolin Enterprise). Mhe. Balozi aliwapongeza Primia Enterprises kwa kuchangamkia fursa za kibiashara zilizopo nchini Rwanda.


