Katika kuhitimisha ziara yake ya kikazi Kigali, Rwanda Mhe January Makamba aliutembelea Ubalozi pamoja na kungalia viwanja vinavyomilikiwa na serikali vilivyopo eneo la Kiyovu na Kacyiru mjini Kigali. Aidha, Mhe Makamba alikutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Jumuia ya Watanzania (Diaspora) ambapo alipokea mawazo ya namna Serikali ya Tanzania na Rwanda zinaweza kufanya ili kuboresha ushirikiano wa pande zote mbili.



