Mhe. Rais Kagame ampokea Mhe January Makamba, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.  Mhe. Makamba yupo nchini Rwanda kwa ziara ya kikazi ya siku nne. ambayo inalenga kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na Rwanda katika sekta mbalimbali ikiwemo Biashara, Nishati na Miundombinu.