Balozi wa Tanzania nchini Rwanda, Mhe. Mej. Jen. Ramson Godwin Mwaisaka, awatembelea wafanyabiashara wa Tanzania wanaoshiriki maonesho ya Kimataifa ya Biashara nchini Rwanda. Maonesho hayo yameanza tarehe 25 Julai, 2024 na yanatarajia kumalizika tarehe 15 Agosti, 2024.





