Leo Tarehe 04 Juni, 2024 Shule ya Msingi ya Reimeta English Medium kutoka Mpanda, Katavi Tanzania imetembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Rwanda kwa lengo la kujifunza masuala mbalimbali yanayotekelezwa na Ubalozi na kufahamu zaidi majukumu ya msingi ya Balozi za Tanzania nje ya nchi.