Mhe. Mej. Jen. Richard Makanzo akutana na wanafunzi wanosoma Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Rwanda ambao ni wanachama wa Chama cha Ukuzaji Kiswahili Rwanda (CHAUKIRWA). Chama hicho kilianzishwa na Wanafunzi hao Chuoni kwao kwa lengo la kuendeleza matumizi ya lugha ya Kiswahili nchini Rwanda. Wanafunzi hao ambao ni Wanyarwanda wengi wao hawajahi kutoka nje ya Rwanda lakini wanazungumza Kiswahili fasaha na wanaendelea kujifunza katika ngazi mbalimbali Chuoni hapo. Aidha Wanafunzi hao wameahidi kufanya juhudi mbalimbali kukiendeleza Kiswahili  na Mheshimiwa Balozi ameahidi kuwapatia ushirikiano ili kufanikisha malengo ya ya kukuzaza Kishwahili.