Balozi wa Tanzania Nchini Rwanda, Mheshimiwa Meja Jenerali Ramson Godwin Mwaisaka amewasili kituoni na tarehe 17 Oktoba, 2023 aliwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho kwa Mheshimiwa Clementine Mukeka, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Rwanda.