Balozi wa Tanzania Mhe. Ernest Mangu amewasilisha hati za utambulisho kuwa Balozi wa Tanzania nchini Rwanda kwa Mhe. Paul Kagame, Rais wa Jamhuri Rwanda tarehe 02 Juni, 2018.

Mhe. Balozi Mangu ameahidi kuimarisha zaidi Ushirikiano uliopo kati ya Rwanda na Tanzania ikiwa ni pamoja na kufanya juhudi za kuimarisha mahusiano ya kibiahara na kiuchumi baina ya rwanda na Tanzani kwa faida ya wananchi wa nchi hizi mbili.