Rais wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli na mwenyeji wake Rais wa Rwanda, Paul Kagame na wananchi wa nchi hiyo, wameshiriki katika tukio maalum la maadhimisho ya miaka 22 ya mauaji ya Kimbari ambayo yalipelekea kusababisha vifo zaidi ya watu Milioni moja nchini humo.

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli...
  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiweka shada la maua wakishuhudiwa na wenyeji wao Rais Paul Kagame na Mama Janeth Kagame wakiweka shada la maua katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mauaji ya Kimbali mjijini Kigali, Rwanda, leo.
  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwa na wenyeji wao Rais Paul Kagame na Mama Janeth Kagame wakiwasili katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mauaji ya Kimbali mjijini Kigali, Rwanda, leo katika maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 22 ya mauaji hayo yaliyotokea mwaka 1994 ambapo watu takribani milioni 1,000,000 waliuawa.