Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha Balozi mpya wa Tanzania nchini Rwanda, Mhe. Ali Siwa. Hafla hiyo ilifanyika, Ikulu, Dar es Salaam tarehe 09 Septemba, 2014.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John Haule (wa kwanza mstari wa mbele) pamoja na wageni waalikwa wakifuatilia tukio la kuapishwa kwa Balozi mpya wa Tanzania nchini Rwanda.
Balozi Siwa akisaini Hati ya Kiapo mbele ya Mhe. Rais Kikwete
Mhe. Rais Kikwete akimkabidhi vitendea kazi, Balozi Siwa.
Mhe. Rais Kikwete akimpongeza Balozi Siwa mara baada ya kiapo.
Mhe. Rais Kikwete katika picha ya pamoja na Balozi Siwa.
Mhe. Rais Kikwete na Balozi Siwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue.
Mhe. Rais Kikwete katika picha ya pamoja na Familia ya Balozi Siwa.
