Jumla Washiriki 440, wanafunzi 365, Walimu na Viongozi 75 kutoka shule za Msingi na Sekondali wakiongozwa na Mheshimiwa Naibu Katibu Mkuu OR-TAMISEMI Dkt. Charles E. Msonde wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mashindano ya michezo kwa Wanafunzi wa Nchi za Jumuiya ya Afika Mashariki - FEASSA yanayofanyika hapa Rwanda kuanzia tarehe 17-28 Agosti, 2023. Tanzania inashiriki katika michezo ya Soka, Mpira wa Kikapu, Mpira wa Wavu, Hockye, Tennis, Riadha, Mpira wa Mikono na Netball.




