Kufuatia Kifo cha Mhe. Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa Awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kilichotokea tarehe 29 Februari, 2024, Wageni mbalimbali wakiwemo Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao nchini Rwanda na Diaspora wameendelea kujitokeza kutoa salamu zao za pole kwa Serikali na Watanzania kwa ujumla tarehe 6 Machi, 2024.








